kwamamaza 7

Kisanduku cheusi cha data cha ndege ya Urusi chapatikana

0

[ad id=”72″]

Kisanduku kinacho tumika kurekodi data cha ndege ya kijeshi ya Urusi iliyoanguka Jumapili iliyopita katika Bahari Nyeusi ikiwa na watu 92 ndani yake kimepatikana.

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Urusi, kisanduku hicho kitasafirishwa kupelekwa Moscow kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi na wataalamu.

Wizara hiyo pia inasema miili ya watu 12 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo pamoja na vipande vya mabaki 156 tayari vimepatikana.

Duru zinaarifu kuwa miili iliyopatikana itasafirishwa kupelekwa Moscow kwa ajili ya utambuzi zaidi.

Ndege hiyo ya kijeshi iliyokuwa inawasafirisha zaidi ya waimbaji 60 wa kwaya ya jeshi la Urusi inayotambulika kimataifa ilikuwa ikielekea katika kambi ya jeshi ya Urusi nchini Syria ilipo anguka kwenye pwani ya mji wa Sochi.

Serikali ya Urusi imekanusha uwezekano wa ndege hiyo kuanguka kutokana na sababu za ugaidi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.