kwamamaza 7

Kirehe: Raia wanaomba msaada kwa sababu ya chawa wa misitu

0

Raia wakaazi wa tarafa za Nyarubuye na Mpanga katika wilaya ya Kirehe, wanaomba msaada wa kupambana na vidudu vya chawa wa msitu ambao wanawakera, wanasema kwamba vidudu hawa wanaumiza kuliko chawa wa mavazi.

Kawaida chawa wa mavazi husababishwa na uchafu kama wanavyokiri raia hawa. Wanasema pia kwamba hakuna raia ambaye anaugonjwa wa vidudu hawa kwa sasa.

Twizerimana Theogene ni moja wa raia wanaosema wanakabiliwa na vidudu hawa.

Alisema “ vidudu hawa ambao hujulikana kama chawa wa misitu, hufanana sana na chawa wa kawaida na hukaa mitini na hujitokeza wakati wa jua. Vidudu hao hushambulia mtu anapopita karibu na mti”.

Alisema zaidi “viongozi wanapaswa kututafutia dawa za kupambana na vidudu hawa kwa kuwa wangetuambukiza hata maradhi mbalimbali ya ngozi kwa sababu wapomdunga mtu huumia sana ngozi”.

Wanafunzi pia wanasema kuwa vidudu hawa huwadunga wanapopita wakienda shuleni.

Alisema “ Vidudu hawa hutushambulia tunapopita njiani tukienda shuleni .Wakati mmoja unawaona wavulana wakivua mashati kwa kusaka vidudu hao wanaowauma na kwa upande wa wasichana inakuwa matatizo sana kwa kuwa si rahisi kwao kujivua wakiwa njiani”

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Tulimtafuta kwenye simu Katibu Mtendaji wa tarafa la Nyarubuye ila simu yake iliitikwa na Kiongozi anejadili masuala ya Kiraia, Jean de Dieu Uwamahoro.

Alisema kwamba katika mikutano ya kila siku wanajadili suala la chawa hawa na wamekwisha toa tarifa kwenye ngazi za wilaya na wanasubiri hatua zitakazochukuliwa”

Ingawa Kiongozi huu amesema kuwa walitoa taarifa kwenye ngazi za wilaya, meya wa wilaya ya Kirehe, Muzungu Gerard, alisema kwamba suala hilo ni lipya kabsa bali tu watatafuta njinsi ya kulijadili na kuchukua hatua.

Amesema “ tumekuwa tukidokezewa kuwepo kwa tatizo hili katika maeneo mengine katika siku za hivi karibuni hatukujua kwamba tatizo hili limefikia hata wilaya yetu, lakini tutalijadili na tulichukulie hatua”

Tatizo la vidudu wa chawa limekuwa likigusiwa kama gumu dhidi ya wakaazi wa karibu na misitu katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Rwanda.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.