kwamamaza 7

Kiongozi wa UN anaomba Dunia kutoa fundisho kwa yale yaliyo tendeka Rwanda

0

Katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres, alitoa tangazo jioni ya ijuma kuhusu uwasiliano na Wanyarwanda katika kipindi hiki cha kumbukumbu la ukumbusho wa mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi kwa mara ya 23.

Antonio Guterres alishukuru hatua ambayo Wanyarwanda wamefanya baada ya mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi, akisema upande wake katika Umoja wa Mataifa ni kufanya iwezekanayo ili mauaji ya kumaliza watu wengi yasiweze kuwa tena.

Katika tangazo hilo katibu mkuu wa UN alisema kuzuia mauaji ya Kimbari ni uajibu wa kila mtu, akisema kuwa mauaji na mengine hayajileti hata kama hufanywa na kundi la watu wachache.

Bwana Antonio Guterres alisema tena mpango wa UN ujulikanao kama Human Rights Up Front huhusika na kusaidia kwa haraka wakati ya mauaji ya Kimbari na kuonyesha mahali kunapo dalili za mauaji hayo.

Aliendelea na kusema kwamba atatia mbele masamaha na kuheshimu haki za binadamu kwa hali ya juu ili watu waishi bila wasi wasi kama vile husema sauti ya Marekani.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alipata muda wa kutoa uito kwa mataifa ili waweze toa fundisho kwa yale yaliyo fanyika Rwanda ili waweze jenga siku zijazo za kiumutu, kuvumiliana na kuheshimi haki za binadamu.

Wanaopendelea bwiza.com iwatembelee na kuwatangazia habari kwenye bidhaa vyao wanaweza kutumia ujumbe kwenye barua pepe ya meckypro@gmail.com, ama wapigie simu kwenye nambari ifuatayo: 0784685981.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.