kwamamaza 7

Kiongozi makamu wa timu ya Rayon Sports akamatwa

0

Kiongozi makamu wa timu ya Rayon Sports,Denis Gacinya amekamatwa na polisi baada ya ombi la kufanyiwa upelelezi liliotolewa na mwendeshamashtaka.

Taarifa hizi zimehakikiswa na msemaji wa  Polisi ya Rwanda,ACP Theos Badege alipozungumza na  chombo cha habari Ruhago yacu.

Afisa huyu amesema kuwa Denis Gacinya amekamatwa ila mengi zaidi kuhusu jambo hili yaweza kuulizwa mwendeshamashtaka.

Gacinya amekamatwa baada ya tume kwa wajibu wa kufanya ufuatiliaji wa matumizi mali ya umma bungeni(PAC) kuwaomba viongozi wilayani Rusizi na mwendeshamashtaka kumfanyia ufuatiliaji baada ya kulipwa fedha zaidi ya kazi aliyoifanya kwenye soko la serikali alilopata.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Inasemekana kuwa Gacinya kupitia kampuni yake kwa jina la MICON,wilaya ilimlipa frw miiyoni 495 badala ya kulipwa frw miiyoni 253.

Bw Denis Gacinya ni afisa wa tatu kutoka timu ya Rayon Sports ambaye amekamatwa na polisi baada ya kiongozi wa muungano wa Rayon Sports,Vedaste Kimenyi na Kochi wa timu hii,Olivier Karekezi.  

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.