kwamamaza 7

Kikosi cha timu ya soka ya Rwanda kuelekea Central Afrika

0

Leo hii meneja mkuu wa timu ya soka ya Rwanda, Antoine Hey ametangaza kikosi ambacho kitasafiri kwenda kucheza na Central Africa( Nchi ya Afrika ya Kati) katika michuano ya kuwania tikiti ya kufuzu michezo ya AFCON 2019 ambayo itachezewa nchini Kameruni.

Akitangaza kikosi hiki wachezaji 19 miongoni mwa 25 waliokuwa katika mazoezi na wengine 7 kuachiliwa huku akisubiriwa kufanya chaguo la mwisho kuhusu mmoja ambaye atabaki kabla ya timu kupanda ndege kwenda Central Afrika.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Makipa :Ndayishimiye Eric Bakame (Rayon Sport), Nzarora Marcel (Police FC) na Kwizera Olivier (Bugesera FC)

Mabeki : Bayisenge Emery (KAC Kénitra),,Rusheshangoga Michel (APR FC), Imanishimwe Emmanuel (APR FC), Manzi Thierry (Rayon Sport), Nsabimana Aimable (APR FC) na Nirisarike Salomon (AFC Tubize, u Bubiligi)

Viungo wa kati: Niyonzima Haruna (Young Africans, Tanzania), Iranzi Jean Claude (MFK Topvar Topoľčany, Slovakia),Mugiraneza Jean Baptiste (Gor Mahia, Kenya), Omborenga Fitina (MFK Topvar Topoľčany, Slovakia), Nshuti Dominique Savio (Rayon Sport), Djihad Bizimana (APR FC) na Niyonzima Olivier (Rayon Sport)

Washambuliaji :Usengimana Dany (Police FC), Tuyisenge Jacques (Gor Mahia, Kenya),Sugira Ernest (AS Vita, DR Congo),

Kikosi hiki kitakuwa kwenye camp mpaka tarehe 8 juni ambapo timu itasafiri kwenda Bangui kucheza na Nchi ya Afrika ya Kati.

Mwa walioachwa ni pamoja na : Rucogoza Aimable (Bugesera Fc), Iradukunda Eric (AS Kigali), Mugisha Gilbert (Pepiniere Fc), Mico Justin (AS Kigali), Niyonzima Ally (Mukura VS) and Kalisa Rashid (MFK Topvar Topoľčany, Slovakia

Timu ya Rwanda iko kanda H pamoja na timu ya Ivory Coast, Guinea na Central Africa ambopo timu ya kwanza kwenye ukanda itafuzu tiketi ya moja kwa moja kwenye AFCON pamoja na timu tatu bora zitakazoshika nafasi ya pili na hata Kameruni.

Mechi hii itapigwa tarehe 11 saa 15 kwa saa za nyumbani kwe Stade Barthelemy Boganda mjini Bangui.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.