Swahili
HABARI

Kigali:Watu wanne wafariki, wengine hawaoni juu ya kunywa pombe

Watu wanne ambao ni wakazi wa kijiji cha Ruliba,tarafa ya Kigali, mjini Kigali  jana tarehe 4 Aprili 2018 wamefariki wengine watatu macho yao yameanza kushindwa kuona.

Mmoja miongoni mwa watu kumi waliokunywa hiki kinywaji cha bei ya frw 300 ametangaza kuwa  walipokunywa walimuambia mfanyabiashara kuongeza utamu katika pombe ila yeye akaongeza wanachofikiri kuwa ni sumu.

“Tulipokuwa tukinywa tuliona shingo lake limeanguka tukampeleka hospitalini ila akafariki tulipokuwa njiani”.

Mwenyeji wa baa ameeleza kuwa kawaida alikuwa akiuza pombe ya kawaida lakini alikuenda kununua kinywaji kingine kwa jina la Kanyanga ili kuongeza utamu wa kinywaji kama wateja walivvyomuomba.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Kwa kawaida nilikuwa nikiuza pombe ya ndizi,nilinunua ‘Kanyanga’ nikachanganya kisha watu  wakiwemo mama na ndugu zangu wakafariki”

“Mtu anakufa anapokunywa  30ml tu” ameongeza

[xyz-ihs snippet=”google”]

Daktari wa magonjwa ya mwilini kwenye hospitali ya CHUK,Dkt. Eric Rutaganda amehakikisha kuwa kulikuwa sumu katika kinywaji hiki.

Msemaji wa polisi mjini Kigali,SSP Emmanuel Hitayezu ametangazia Ukwez.comi kuwa polisi imeanza upelelezi na kuwa atabidhiwa yeyote atakayeonekana kuwa na uhalifu.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

[xyz-ihs snippet=”google”]

 

 

 

 

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com