kwamamaza 7

Kigali:Waendesha pikipiki walalamikia unyonyaji wa vyama vya ushirika

0

Waendesha pikipiki wa mjini wa mjini Kigali wametangaza kulalamikia huduma za unyonyaji unaofanywa na vyama vya ushirika vyao.

Mmoja wao ametangazia VOA kwamba hajawahi kuona manufaa ya ushiriki wake katika chama cha ushirika kunyume na fedha wanazolipa kila siku ambazo viongozi wao hawatowi maelezo ya matumizi yake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Sijaona umuhimu wa kuwa na chama cha ushirika ila kinachonifanyia ni unyonyaji tu”amesema.

Mwenzake ameongeza kwamba wanalipa fedha kila siku lakini viongozi wa vyama vya ushirika hawaelezi usimamizi na matumizi ya fedha hizi miaka nenda rudi.

Mimi hulipa elfu tisa kila mwezi ila sijawahi kunufaika kwa fedha hizi”ameongeza.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mmoja mwa viongozi wa vyama vya ushirika hivi ambaye hakutaka majina yake kutambulika amesema kuwa serikali ndiyo chanzo cha kisa cha kuwanyonya waendesha pikipiki hawa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Tunakumbwa na hasara kwa kuwa serikali inatupatia mzigo unaozidi uwezo wetu,tunajikuta katika hasara nasi tukawanyonya kwa kujaza pengo”ameleza.

Mkurugenzi wa Ofisi ya maendeleo ya vyama vya ushirika(RCA),Gilbert Habyarimana amesema kuwa kuna vyama vya ushirika ambavyo vinafuata mwendo wa zamani na kuwa  kunatarajiwa kuboresha kanuni na kukumbusha kuwa hata kama si asilimia mia kuna hatua iliyopigwa .

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya sheria ya 2007 husika na vyama vya ushirika,makala yake 27 inandikwa kwamba washiriki wa chama cha ushirika hawana budi kufanya mkutano mala mbili kila mwaka ili kuhojiana kuhusu hali ya chama cha ushirika,kinyume na madai ya waendesha pikipiki wanaosema kuwa wanamaliza miaka miwili bila mkutano.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kulisikika mala nyingi malalamishi ya waendesha pikipiki nchini kote wakisema kuwa fedha wanazo kusanya zinanufaisha viongozi wao.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.