kwamamaza 7

Kigali:Mtangazaji akimbilia nje ya nchi

0

Mtangazaji wa Radio Flash Fm,Etienne Besabesa amekimbilia nje ya Rwanda.Huyu ametangaza kwamba ni  juu ya sababu za kazi yake ya utangazaji.

Kinyume na aliyoyatangaza,viongozi wa Flash Fm wameleza kuwa Besabesa alifukuzwa kazini mwezi Julai na wengine kueleza kwamba anadhamiria kupata hati za hali ya ukimbizi nchini Kanada.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Besabesa ametangaza kuwa alikimbia kwa kuwa aliona kwamba maisha yake yalikuwa hatarini kwa sababu za kazi zake.

Nilikimbia kwa kuwa niliona maisha yangu yalikuwa yanakaribia kuwa hatarini juu ya kazi yangu ya utangazaji”amesema mtangazaji Besabesa.

Pia ameongeza kwamba alitishwa na viongozi wa mitaani baada ya kutangaza habari husika na nyumba zilizokuwa zikibomolewa ila zilizogengwa kwa rushwa zilizoko mjini Kigali.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwenyekiti wa Radio Flash,Louis Kamanzi amesema kuwa huyu hakuwa mfanyakazi wake kuanzia mwezi Julai na kuwa hajui kuhusu habari  iliyoleta mzozano.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Watangazaji wenzake wamesema kuwa amekimbia kwa sababu zake binafsi.

Besabesa aliwahi kufungwa gerezani nchini Burundi mnamo mwaka 2015.Huyu amekimbilia nchini Uganda atakapondoka kuelekea Afrika Kusini na kuenda Kanada.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.