Mahakama kuu mjini Kigali leo tarehe 7 Meyi imehairisha kesi ya Diane Rwigara na mama mzazi wake Adeline Rwigara Mukangemanyi wanaotuhumiwa uchochezi.

Mahakama imeamua hili baada ya mwanasheria wa Adeline Mukangemanyi Rwigara, Me Gatera Gashabana kuelezea mahakama kwamba ana kesi nyingine mahakama ya juu leo.

Diane Rwigara(kushoto) na mama mzazi wake Adeline Mukangemanyi/Picha na Intaneti

Mwanasheria wa Diane Rwigara,Me Buhuru Celestin  amesema hakuna tatizo lolote la kutotii hili ombi la mwenzake.

Kwa hili,Jaji Ndibwami ameamua kuhairisha hii kesi.

Diane Rwigara aliyewania ugombezi wa rais mwaka 2017  anashtakiwa uchochezi,matumizi ya hati bandia pamoja na Adeline Mukangemanyi anayeshtakiwa  uchochezi,ubaguzi wa kikabila.

Kesi hii itaendelea tarehe 22 Meyi 2018

Subscribe to BWIZA TV to get news and song update

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina