kwamamaza 7

Kigali:Dereva akamatwa na polisi baada ya kushtakiwa na wasafiri juu ya matumizi ya simu wakati wa kuendesha gari

0

Wasafiri wamemripoti dereva wa kampuni ya Usafirishaji mjini Kigali,Emmanuel Ndereyimana kuhusu matumizi ya simu ya mikononi wakati wa kuendesha gari kutoka Kayonza-Kigali.

Msemaji wa polisi  wa idara ya Trafiki na usalama barabarani,CIP Emmanuel Kabanda amehakikisha taarifa hizi kwa kusema kuwa huyu amekamatwa baada ya polisi kupokea simu kadhaa za wasafiri pamoja na waendesha miguu wakijulisha jambo hili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Kwa mjibu wa wasafiri,dereva huyu alikuwa akiendesha gari kwa mkono mmoja mwingine ukitumia simu,aliposhauriwa kuachia hapo akakataa kwa uhasama kisha akamuacha njiani mmoja mwa wasafri aliyekuwa akielekea mjini Kigali”amesema CIP Kabanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

CIP Emmanuel Kabanda akizungumza na The New Times, ameongeza kuwa hawatakubali tabia hizi kuendelea na kuwa wanafurahi kwa kuwa wasafiri wamezinduka kuhusu haki zao.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya Polisi ya nchi (RNP) kuanzisha kampeni za usalama wa barabarani kwa kusisitiza ule wa waendesha miguu ambao mala nyingi ni wathiriwa wa ajali za barabarani.

Baadhi mwa ajali kubwa za barabarani kuanzia mwezi wa Ogasti hadi October asilimia 46% zilikuwa za waendesha miguu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.