Swahili
Home » Kigali: Watatu wajeruhiwa kwa ajali ya moto katika gereza la 1930
HABARI MPYA USALAMA

Kigali: Watatu wajeruhiwa kwa ajali ya moto katika gereza la 1930

Majeruhi tatu wameripotiwa kutoka ajali kali ya moto katika gereza maarufu la Kigali lijurikanalo kama 1930. Ajali hio ilipatikana jana mchana kwenye sikukuu ya Krismasi na waziri wa sheria pamoja na kiongozi wa polisi walifika na kutoa maelezo, ijapokuwa asili ya moto haikujulikana bado.

Kiongozi wa shirika la kuzima moto katika polisi ya Rwanda, ACP John Baptist Seminega aliambia wandishi wa habari, baada ya ajali kwamba sababu ya moto haijajulikana. Alieleza tena kuhusu sauti za lisasi zilisikika kama fununu zilisema kwamba waliwapiga lisasi wafungwa kwa kuwazuia kutoroka.

‘’Hakuna mfungwa hata mmoja amepigwa lisasi, isipokuwa wafungwa watatu wamejurihiwa. Wafungwa wawili wajeruhiwa zaidi lakini hawakuuguzwa na moto bali wamejeruhiwa wakati wa kukimbia kwa kuokoa maisha wakielekea nje. Hakuna kupigwa lisasi.’’ Seminega alikataa.

img_1714
Kiongozi wa shirika la kuzima moto katika polisi ya Rwanda, ACP John Baptist Seminega

Viongozi kadhaa serikalini walifika kwenye eneo la tukio wakiwemo mawaziri na wakuu wa jeshi na polisi pamoja na magari ya kuzima moto yalifika mapema.

Waziri wa sheria Johnston Busingye alisema eneo iliyoteketea ni takribani mita 20 na mali iliyoharibika ni chache kama vitanda vya wafungwa. Alisema kwamba mfungwa mmoja alijeruhiwa zaidi wakati wawili wengine wajeruhiwa wakati wa kuokoa maisha.

abanyururu
Mwanzoni wafungwa walipanda ua wakijaribu kutoroka

Kuhusu sauti ya lisasi, Busingye alieleza. ‘’Kuna wafungwa walijaribu kupanda ua ili waweze kutoroka ndipo kupiga lisasi hewani ili kuwazuia. Hakuna mtu afarikia katika ajali hii ya moto.’’

img_1725
Waziri wa sheria Johnston Busingye

Gereza hili linahifadhi wafungwa wa mchanganyiko wale wa kisiasa na wengine wa mauaji ya kimbari. Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa Ni Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka 4 iliyopita Kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia.

 

img_1690
Wafungwa walibaki ndani baada ya kuzuiwa kutoroka
img_1692
Magari ya kuzima moto ya polisi yalifika mapema

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com