kwamamaza 7

Kigali: Wajuzi wa wilaya pamoja kwa kupinga ughaidi

0

Wajuzi wa kupiganisha ughaidi kutoka polosi za wilaya na jamii za kimataifa wapo kwenye mkutano wa siku mbili Kigali na wakiwa na lengo la kujifunza kwa pamoja namna ya kuzuia kinacho vamia usalama siku hizi.

Mkutano huo umeshiriki zaidi ya nchi kumi pakiwemo vingozi wa polisi katika bara la Afrika jumuia ya mashariki, (EAPCCO) na wasimamizi kimataifa Interpol pamoja na Institute of Security Studies  (ISS) katika mkutano ulio anza tarehe 21 Februari 2017.

Kiongozi makamu wa polisi ya Rwanda anaye huhusika na uongozi na wafanya kazi, DIGP Juvénal Marizamunda akiwa mtume maalum, kwa kuanzisha mkutano alisema ya kuwa mkutano kama huu ndio wa muhimu kwa kujenga mipango ya kupiganisha ughaidi katika wilaya na kimataifa.

DIGP Marizamunda eti:” nguvu zinazo fanya kupinga ughaidi ili utoe malimbuko itatokana na juhudi ya kila nchi”.

Wajuzi wanasema ya kuwa ughaidi uliendelea tangu miaka nenda, hesabu European Institute for Security Studies, husema ya kuwa mwaka wa 2015, zaidi ya watu 11.000 walipoteza maisha  Somaliya, Kenya, Sudani, Sudani Kusini na Etiyopiya.

Waghaidi wa wilaya ni katika makundi ya “Al-Shabab ,ADF Naru na FDLR, ISIS na Al-Qaeda”

Francis Muhoro , anaye ongoza kamati ya EAPCCO , alisema ya kuwa katika wilaya, iwe nchi moja ao nchi jirani ambayo husaidiana kwa kupiganisha wanamgambo ili kuzuia wanaofundisha ughaidi na kuwakosesha wafuasi.

Hadi sasa Kenya kuna kituo maalum kwa kupiganisha ughaidi wakiwa pamoja na Interpol kwa kusaidia nchi za EAPCCO, wakipewa mafundisho kwa kupiganisha ughaidi, makosa ya teknolojia na makosa ya kimaendeleo haraka.

Mwakilishi wa Canada katika nchi ya Rwanda, Yannick Hingorani, alisema ya kuwa Canada ni nchi ambayo ilisaidia nchi za wilaya kupanisha ughaidi na hata kamwe haitachoka kuwasaidia katika vitendo vya kupinga ughaidi.

Willem Els mtume kutoka ISS, eti:” hatuna kuchagua,… sherti tuwasiliane kwa kuwa pamoja, kwa kuwa kundi hizo za ughaidi zinazidi nguvu nchi moja moja wakiwa peke yao”.

Mkutano wa tatu wa EAPCCO kwa ajili ya ughaidi huja baada ya ingine iliyofanyika Seishele mwezi Februari 2014, na ingine iliyo fanyika mjini Naivasha nchi ya Kenya mwezi mach mwaka nenda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.