kwamamaza 7

Kigali: Mtumishi wa nyumbani awapa sumu wanafamilia na kuiba fedha

0

Familia ya Innocent Mugabo inamtafuta msichana aliyekuwa mtumishi wa nyumbani kwa kuwapa sumu watoto wake na mke wake.

Haya yalitokea baada ya msichana huyu kuwapa maziwa yaliyokuwemo sumu wakati wa asubuhi alipokuwa akiwasaidia kujianda kwenda shuleni na kuwachunga akamwaga sumu kwenye maziwa yao.

Bwana familia yule anayetambulika kwa jina la Innocent Mugabo alijaribu kuwapa usaidizi wa moja kwa moja kwa kuwa walikuwa wameanza hata kutapika tapika  na kuwapeleka zahanati na wakati huo mtumishi huyo alikuwa amekwisha toroka.

Inasemekana msichana huyo mwenye umri wa miaka 27[ambaye tumependa kutotaja jina lake]  ni raia wa Nyamasheke kwenye tarafa ya Kanjongo. Huyu alitoroka pia na fedha alizochukuwa kwenye mkoba wa mkewe Innocent uliokuwa sebuleni.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Baada ya tukio hilo Innocent Mugabo alipeleka kesi yake kwenye Kituo cha Polisi ya karibu na makazi yake Gikondo na hata kutoa picha kwa kampuni za kusafirisha abiria wa kuelekea wilaya ya Magharibi.

Hata hivyo Mugabo amesema haelewi sababu ya msichana huyo kufanya maovu hayo kwa kuwa alikuwa ana uhusiano mzuri na wanafamilia na kuwatunza watoto kwa kuridhisha.

Kwa sasa taratibu za kumtafuta mhalifu huyu zinaendelea kwa kuwa kumechapishwa matangazo yenye picha anayoonyesha kutafutwa kwa huyo msichana kwa makosa ya kuiba na kuwapa sumu wanafamilia aliokuwa akiwatumikia kazi za nyumbani ili mwenye kumpata aje amkamate.

Hadi sasa picha zake zimeanza kusaamba kwenye mitandao ya kijami.

Tukio kama hili si mara ya kwanza kujitokeza kwenye eneo hili ikiwa si miezi mingi baada ya mtumishi wa nyumbani kumpa sumu Bwanawe ila kwa majariwa aliweza kunusurika.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.