Swahili
HABARI

Kigali: Maji yazidi kuwa hatari kupatikana

Tatizo la ukosefu maji linazidi kuwa hatari kwa wakazi wa tarafa mbalimbali za mji wa Kigali ambapo wanalazimika kukaa miezi kadhaa bila maji licha ya kuwa Shirika la Kusambaza maji la WASAC kuahidi kutolea suluhu kwa tatizo hili kabla ya mwezi Julai mwaka huu.

Maeneo mengi ya mji wa Kigali yamekuwa yakikumba na tatizo la ukosefu maji ambapo wapaswa kukaa miezi mingi bila maji. Sehemu kama Nyamirambo, Nyakabanda, Kanombe na hata maeneo mengine.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mkurugenzi wa shirika hilo la WASAC akijibu maswala ya bwiza.com kupitia mtandao wa twitter kuhusu ukosefu maji amesema kwamba tatizo la maji limetolewa suluhu kwa kiasi fulani na kuongeza kwamba wanaokosa maji kwa muda mlefu ni wenye kuwa na matatizo ya pekee kama kutobokewa kwa mabomba ya maji.

Alipoulizwa kuhusu maeneo yanayoshinda muda mlefu bila maji amesema kwamba wakazi wa maeneo kama Nyakabanda wanaokosa maji kwa muda mlefu wangetafuta ikiwa tatizo si la pekee kama kutobokea na mabomba ya ya maji kwa kuwa wengi wanapata.

Mkurugenzi huo alipoulizwa ikiwa kuna utaratibu wa kugawa na kukagua matumizi ya maji alisema “tunaufanya ukaguzi wa siku kwa siku na panapopatikana tatizo kama kuharibika kwa vyombo vya kusafirisha maji hayo linawekwa kwenye bajeti na hivyo kufanya kuchukua muda mlefu kulingana na uzito wake”

Amesema kuwa pia kuna kiwanda cha maji kinachokaribia kukamilika na ambacho kitatoa maji kwa kiwango cha 105,000 mkitakachosaidia kupatikana kwa maji katika sehemu za mji. Hapa amesema kwamba kuna maeneo yaliyokumbwa na ukosefu maji kama Kanombe,Samuduha na Kimironko ambayo yatashughulikiwa kwenye mradi mpana wa kujenga viwanda vya kutoa maji.

Mkurugenzi wa shirika hili amesema kwamba licha ya kuweko kwa matatizo kama haya kuna hatua kubwa iliyopigwa kutolea suluhu ukosefu maji mjini Kigali kulingana na hali ilivyokuwa miaka iliyopita.

 Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com