kwamamaza 7

Kigali: Mahakama yawaita watu wengine kwenye kesi ya Diane Rwigara na mzazi wake

0

Mahakama kuu mjini Kigali imewaita watu wanne wakiwemo shangazi yake Dianne Rwigara Mugenzi Thabita Gwiza, Mukangarambe Xaverine, Mushayija Edmond maarufu Sacyanwa na  msemaji wa Chama cha Rwanda National Congress,Jean Paul Turayishimiye.

Tangazo la hii mahakakama limeeleza hawa watu ambao hapajulikani wanapoishi wanalazimishwa kufika mahakamani tarehe 24 Julai 2018.

Mkurugenzi wa mahakama Charles Kaliwabo ameeleza hawa watahojiwa kuhusu mashtaka ya uchochezi  kupitia sauti walizozungumza na Diane Rwigara na mama yake kupitia Whatsupp na matumizi ya hati bandia.

Kaliwabo ameongeza  anastahili kuwajulisha yeyote anayewajua.

Haya ni baada ya wanasheria  Diane Rwigara Me Buhuru na wa mzazi wake Me Gatera Gashabana kuomba mahakama kuwafikisha mahakamani  kwani uamuzi wa kesi hii unawahusu.

Inatuhumiwa kuwa wengi mwa hawa wanaishi nchini Canada na Marekani.

Fred Masengeho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.