kwamamaza 7

Kigali: Mahakama yaanzisha upya kesi ya aliyelenga kuwania urais

0

Mahakama Kuu Mjini Kigali imeanzisha upya kesi ya Diane Rwigara aliyelenga kuwania urais mwaka 2017 na mzazi wake  Adeline Rwigara.

Uamuzi huu ni baada ya mahakama kusema kwamba kesi itaendelea bila kujali kwamba kuna watu wengine wanaostahili kuonekana kizimbani kwenye kesi hii.

Mwendeshamashtaka  Ndibwami Rugambwa ameeleza  anamshtaki Adeline Rwigara kugawa watu kikabila na uchochezi.

Pia, huyu ameelezea mahakama Diane Rwigara anashtakiwa matumizi ya hati bandia wakati wa kutafuta ugombea wa urais.

Upande wa washtakiwa wamesema hawakubali haya mashtaka yote.

Pengine, mwendeshamashtaka amesema kuna watu wengine wanne wakiwemo Tabita Gwiza ( Shangazi ya Diane Rwigara) Mukangarambe Saverina, Mushayija Edmond maarufu kama Sacyanwa na Jean Paul Ndayishimiye ambao watahukumiwa bila kuwepo.

Wanasheria wao wametangaza wamesikia mashtaka ambayo hawayakuyasikia baada ya kukamatwa kwa wateja wao kama vile sauti za mazungumzo na hawa watu wanne amabao wengi mwao wanaishi nchini Canada na Marekani.

Mahakama imeamua kesi hii itaendelea baada ya siku 60.

 Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.