kwamamaza 7

Kigali: Kiongozi wa tarafa ya Muhima ametiwa mbaroni kwa hutuma ya kuomba rushwa

0

John Ruzima katibu mtendaji wa tarafa ya Muhima, wilaya ya Nyarugende alikamatwa na polisi ya Rwanda tarehe 22 Mach 2017 akishutumiwa kuomba rushwa.

SP Hitayezu Emmanuel, msemaji wa polisi ya Rwanda mjini Kigali eti “ni kweli anafungiwa akishutumiwa kuomba na kupokea zawadi ao mambo mengine kinyume na sheria”, hivi yupo kwenye stesheni ya Kimihurura, wilaya ya Gasabo, mjini Kigali.

Taarifa husema ya kwamba wakaaji walisema mengi kuliko wakisema ya kuwa aliwanyanyasa.

Mke mmoja wa Nyabugogo eti “ alipenda pesa sana, kila mwezi aliomba msaada”. Aligusia hata pesa zinazo ombwa raia kwa ajili ya kuuza gari la msako, eti “hivi tunaombwa pesa ya kuuza gari ya msako tena tulionyeshwa pikipiki saba zinazo husika na msako wa usalama”.

Wenye kuwa na bar za kuuzisha pombe wana saa za kufungua na kufunga, wanafungua saa saba na kufunga saa inne za usiku, ukidanganyika hata dakika chache alikuwa akikuomba kati ya pesa za Rwanda 50.000 na 100.000.

Raia mmoja ametoa mfano ya bar walio toa pesa hizo kama bar Bishushe, Cool Garden na kwa Innocent.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa kuwachosha hata katika kila bar walilazimishwa kulipa mhusika na usalama wa kike na kiume kwa kusaka, na wanajiswali namna gani wanafungua saa chache na kulipa wahusika na msako elfu 200 kila mwezi, bila kusahau kodi na ushuru, hata faida kwa mfanya biashara ni gani?

Raia husema pia kwamba waliombwa rushwa wakati wa majenzi, na aliye toa taarifa anasema kwamba hata kama yeye hakutoa anafahamu wengine waliotoa pesa hizo, mwengine eti “hizo sherehe za kila siku hakuna anayejua msaada hata hesabu ya pesa na matumizi, tunaona hema na wanamziki nasi tunaburudika”.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.