Swahili
Home » Kigali: Kesi ya wanaoshtakiwa kupindua serikali yahairishwa
HABARI MPYA

Kigali: Kesi ya wanaoshtakiwa kupindua serikali yahairishwa

Mahakama Kuu mjini Kigali jana tarehe 9 Julai 2018   imehairisha kesi ya wanachama 11 cha FDU-Inkingi ambao wanatuhumiwa mashtaka yakiwemo kulenga kuipindua serikali ya Rwanda.

Mahakama imeamua baada ya mmoja mwa washtakiwa kwa majina ya Erneste Nkiko kukosekana mahakamani, jambo ambalo limezusha changamoto ya fikra mahakamani kwa upande wa wanasheria na wa mwendeshamashtaka.

Wanasheria  Me gatera Gashabana na Me Antoinette Mukamusoni wameeleza kesi inaweza kuendelea bila kusubiri Nkiko Erneste.

Hata hivyo, mwendeshamashtaka amesema haiwezekani kwani wote wanashtakiwa uhalifu unaofanana na ni umuhimu wote kuonekana kotini .

Jaji kwenye kesi hii, baada ya kusikiliza pande zote husika, ameeleza kesi hii itaendelea tarehe 30 mwezi huu.

Wanachama wa FDU-Inkingi wanashtakiwa kuunda kundi la jeshi kinyume na sheria na kuungana mkono na wanamgambo wa FDLR nchini DR Congo.

Wanakubali kuwa wanajua kamati la vyama vikiwemo ‘Rwanda National Congress’ la jen. Kayumba Nyamwasa.

Isisahaulike  kuwa Mwenyekiti wa Chama cha FDU, Ingabire Umuhoza Victoire alihukumiwa kufungwa miaka 15 juu ya upuuzaji wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com