kwamamaza 7

Kigali: Kesi ya Diane Rwigara, nduguye na mzazi wao yahairishwa tena

0

Kesi ya familia ya Diane Rwigara,nduguye Anne Rwigara na mama mzazi wao ,Adeline Mukangemanyi  leo imehairishwa kwa mala ya pili.

Huu ni uamuzi wa mahakama ya Nyarugenge baada ya mwanasheria wa watuhumiwa Me Buhuru Pierre Celestin kueleza kwamba hakuona hati za kesi ya wateja wake baada ya kuikosa kwenye intaneti kwa hiyo akapendekeza kuahirisha kesi hii.

Mwanasheria huyu ameleza kuwa wanahitaji kuona hati hizi ili  wateja wake waelewe uahalifu wanaoshtakiwa kwa kuwa wamesema kwamba hawajajua bado uhalifu wanaotuhumiwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Diane Rwigara anashtakiwa kutumia hati bandia ili aweze kuwania uchaguzi wa rais na uchochezi,nduguye Anne Rwigara anashtakiwa kuzusha ghasia nchini pamoja na mama mzazi wao,Adeline Mukangemanyi anayeshtakiwa uchochezi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya kuhairisha kesi hii tarehe 6 Octoba 2017 kwa kukosekana kwa mwanasheria,Me Buhuru Celestin aliyeleza kuwa ana kesi nyingine.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kesi itaendelea jumatano tarehe 11 Octoba 2017.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.