kwamamaza 7

Kigali: Kamanda wa polisi ampiga mwanamke hadi kuperekwa hospitalini

0

Akaniwabo Jacqueline anakuwa katika kituo cha afya cha Kabuye wilayani Gasabo, Kigali kwa sababu ya kupigwa vikali na kiongozi wa polisi na hivi maisha yake yanakuwa hatarini.

Asili ya tukio hii ilikuwa kuwapa habari waandishi wa habari kuhusu mambo ya ukatili ambayo hufanywa na raia mmoja, Niyonsenga Albert. Baada ya kutishiwa na Albert, alienda kwenye kituo cha polisi ili kueleza unyanyasaji hufanyiwa ndipo alipigwa na kamanda wa polisi katika kituo cha Jabana.

“Naumizwa kwa ajili ya habari niliwapa wandishi wa habari wa TV1. Kwa ufupi, mwanamume anayeitwa Niyonsenga Albert amezoea kuwapiga watu kwa niaba ya kuwa na pesa.” Mgonjwa Jacqueline alieleza.

Alisema tena kwamba alishangazwa na kumkuta mshutumiwa Niyonsenga Albert katika kituo cha polisi kisha akapigwa.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

“Nilipekuwa hatua mbili ili kukimbia, kamanda alinishika vile vile na kuniingiza gerezani. Alinipiga ngumi mara mbili nikiwekwa katika mapingu kisha nikaanguka chini, na kunipiga teke gotini.” Alieleza.

Mukamuhanda Seraphine, Kiongozi wa kituo cha afya cha Kabuye ambapo mgonjwa Akaniwabo Jacqueline analala; alisema kwamba Jaqueline alikuwa amepigwa sana.

Msemaji wa polisi ya Rwanda mjini Kigali, Spt Emmanuel Hitayezu; kwa maongezi ya simu na City Radio alisema kwamba hakujua habari za kupigwa kwa Akaniwabo Jaqcueline na kiongozi wa polisi. Alisema kwamba polisi itafuata kesi hio ili kuitatua na kuweka wazi ukweli.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.