kwamamaza 7

Kigali :Gereza ya Gasabo yafungwa milango

0

Baada ya wafungwa 82 ambao walikuwa wanabakia katika Gereza ya Gasabo kuhamishwa katika Gereza ya Nyarugenge tarehe 04 Juni, kwa mujibu wa habari kutoka Ofisi Kuu ya Magereza RCS. Gereza hii imekwisha fungwa milango.

CIP Hillary Sengabo, Spika wa RCS ametangaza kuwa kufungwa huku kumesababishwa na kwamba imejengwa katikati mwa mji ikiwa kuna nyingine ambayo imekwisha jengwa yenye vifaa vyote.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Gereza hii ambayo ilishika moto katika mwezi wa Machi ambapo watu saba walipata majeraha madogo, na kufanya vifaa vyingi kuharibika vikiwemo vya wafungwa ingawa walipewa vingine kama fidia . hata hivyo hiyo haikuwa sababu ya kufungwa kwake.

CIP Sengabo amesema “ Kulikuwa na mpango wa kuifunga gereza hii kwa kuwa imekuwa katikati mwa mji, la pili kuna nyingine ambayo imekwisha jengwa yenye vifaa vyote muhimu”

Baada ya gereza hii kushika moto, wafungwa waliokuwemo walifanya mgomo kwa kurusha mawe na kuni barabarani na kwenye nyumba zaa wakazi jirani, wakati huo RCS ilirusha mabomu ya machozi (tear gas) kuwatawanya wafungwa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.