kwamamaza 7

Kigali :Fujo yazuka Nyabugogo baada ya walinda usalama kumpiga mwendesha biashara ya kutembeza bidhaa

0

Fujo kali iliyokuwemo mapigano yazuka Nyabugogo baada ya walinda usalama wa ngazi za wilaya(DASSO) na wanadoria wa vijiji kumpiga mfanyabiashara ya kutembeza bidhaa katika eneo la biashara la Nyabugogojioni ya Alhamisi tarehe  10 .

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Walioshuhudia mapigano hayo wamesema chanzo chake kilikuwa kumpiga mfanyabiashara ya kutembeza kwa kufeli kuwapa fedha kama hongo na hivyo kuzua fujo la watu waliokuja kushuhudia huko nao wakakijitia katika mapigano haya kwa kumpiga yeyote bila kubagua.

Wananchi waliohojiwa na kituo cha televisheni cha Loyal Tv kilichotangaza habari hii, wamesema kwamba wanateswa sana na utekelezaji kazi wa ngazi hizo za walinda usalama kwa kuwa wanamwonea kila mtu.

“raia mwingine alisema wanaweza hata kumpiga mpita njia hasahasa anapoona walinda usalama hao wakimpiga mtu na kujaribu kuuliza tatizo gani”.

Raia mwingine amedai kuwa walinda usalama hao huwa wanamtoza  faini mtu kwa kutumia stakabadhi ya faini ya magari na wakajiuliza ikiwa wao ni waendesha magari au pengine.

Watembezaji  hawa wanasema kuwa pia kunakuja wakati fulani akafungiwa kwenye vijumba vinavyotumika kama ofisi na kupigwa huku akilazimishwa kutoa hongo na wanapokosa basi hupata taabu.

Ngazi hizi za walinda usalama zimekuwa zikitupiwa lawama na wananchi kwa kutekeleza kazi yao kwa njia zisizostahili kwa kuwa huwa walinda usalama wanaonea kwa sababu zisizo mara nyingi na msingi.

Ingawa meya wa mji wa Kigali alilieleza fujo hiyo kama tatizo ndogo lililozuka kati ya walinda usalama hao na wazunguzaji na ambalo lilimalizwa kwa mara na viongozi wa ngazi husika, msemaji wa polisi ya Rwanda, ACP Theos Badage alisema kwamba tukio kama hilo mpya kabisa na kwamba linastahili mikakati fulani.

 

Spika wa Polisi ya Rwanda THEOS BADEGE

Msemaji huyu amepata fursa ya kuwaonya wafahyibiashara kama hizo kutopigana na walinda usalama kwa kuwa ingechukuliwa kama ukiukaji wa sheria.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.