kwamamaza 7

Kigali Convention Center imenionyesha kua wa Afrika wana uwezo – Rais Kagame

0

Rais Kagame amesema kua jengo la Kigali Convention Center lilijengwa na wa Afrika na ilimuonyesha kwamba ni wajuzi tena waweza kufanya zaidi ya hayo katika bara zingine.

Katika maongezi “Kujenga Afrika” ilio pitika kwenye  televijeni CNBC katika mkutano wa Uchumi ulimwenguni WEF 2017  mjini Davos-Klosters tarehe 18 Januari 2017, rais Kagame aliongelea waafrika namna anavyo ona njia ya maendeleo.

Alisema kua Rwanda inaendelea ni kwa sababu wapo na lengo ya kufanya mema pekee ili historia ya nchi ibadirike, eti: “ ukitamani kujenga nchi sherti utiye sheria na uwe wa kwanza kuyaheshimu. Sherti pawe kielekezo na kutii kanuni na sheria bila  kupita njia panya”.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

kagame kagame3 kagame4

Ni vigumu nchi za Afrika kuendelea kama nchi za bara hilo hawafungui njia za wafanya biashara. Waafrika wenyewe ni vigumu kutoka katika nchi na kwenda katika nchi nyingine, hakuna mabadiriko. Sherti serikali irahisishe njia za wafanya biashara.

Kwa kumalizia rais Kagame amesema waafrika wapo na elimu pia ujuzi wa hali ya juu eti :“niwape mfano rahisi, Rwanda tumeonyesha jengo ambalo lilitwala muda mrefu, nilipochunguza nilikuta wahandisi waliojenga ni waafrika, mmoja wa Rwanda, mwengine ni wa Kenya, mwengine katoka Zimbabwe. Nimegundua kua katika Afrika kuna watu wengi wenye vipao sherti wapewe nafasi ya kutumikisha ujuzi wao.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.