kwamamaza 7

Kigali: Amuua mke wake kwa kisu na kujipeleka kwa polisi

0

Mwendesha piki piki, Thierry Harerimana amemuua mke wake, Josephine Niringiyimana kisha akajipeleka kwenye kituo cha polisi.

Kisha hiki kilitokea juma tatu wiki hii, Harerimana,30, alimdunga kisu tumboni mkewe, Josephine,31, walioishi kinyume na sheria  kisha akapotea.

Katibu Mtendaji wa eneo la Kinyinya, Umuhoza Rwabukumba amehakikisha hizi taarifa kwa kusema “ Alipomaliza kumuua alijifisha lakini baadaye alikuja usiku na kujipeleka kwenye kituo cha polisi.”

“ Wanawe wametuambia baba yao alikuwa amelewa alipofika nyumbani. Alimkaba shingo na kumdunga kisu tumboni.”

Rwabukumba amewataka wakazi wasuane wakiwa na kutoelewana kati yao. Amewahamasisha kuomba msaada wa kutoa suluhisho.

Pia, Msemaji wa Ofisi ya Upelelezi nchini, Mbabazi Modeste,amesema huyu amejileta mwenye kwenye kituo cha polisi na kwa sasa mambo ya upelelezi yameanzisha kufuatia hiki kisa.

Hata hivyo, majirani wao wamesema hakukua ugomvi kati ka familia hii.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.