[ad id=”72″]

Mtu ambaye hujulikana kwa jina la Munyaneza Ignace amekamatwa akijaribu kuuza pikipiki aliyopewa kwa usafirisaji ya watu.

Munyaneza Ignace mwenye umri wa miaka 42 ametiwa mbaroni na polisi ya wilaya Kichukiro akijaribu kuuza pikipiki yenye namba RD472I,  ya aina ya TVS  na hivi yupo stasheni ya polisi katika wilaya hiyo.

Kwa kawaida mwenyeji wa pikipiki hio ni Simpanika Innocent, amesema kwamba pikipiki yake ilikua ikitwaliwa na Munyaneza kwa usafirisaji ya watu, na nyuma akakamatwa akitafuta wateja wa pikipiki hio kwani wakati alipo kua akisafirisha na alikua akitafuta wateja.

Wakaaji ambao walijua pikipiki hio vizuri ndio walijulisha polisi kwamba mtu huo huuza pikipiki isiyo kuwa yake.

Musemaji wa polisi katika mji wa Kigali Superintendent of Police (SP) Emmanuel Hitayezu amehakikisha taarifa hio akisema kwamba mtu huo alikamatiwa katika kata ya Niboye, wilayani Kicukiro na pikipiki ikiuuza elfu 300 pesa ya Rwanda.

Wakati upelelezi huendelea kwa ajili ya mtu huo ambae alitaka kuuza pikipiki isiyo kuwa yake, pikipiki imepewa Simpanika Innocent.

SP Hitayezu ametoa shukrani kwa wakaaji na kuendelea kutoa uito na kusema ni vizuri kutoa taarifa mapema ili kuzuia makosa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.