kwamamaza 7

Kesi ya wakufunzi wa waalimu na REB yazidi kuwa nzito

0

Mahakama Kuu ya Gasabo yaahirisha mkutano wa maandalizi kesi ya wakufunzi wa walimu ambayo wanaishtaki REB kuwafukuza kazi kinyume na sheria. Mahakama ya Gasabo yaahirisha kesi hiyo hadi 27 Septemba kwa misingi ya kuwa hayakuweko maandalizi ya kutosha.

Kesi hii imekuwa ikicheleweshwa kiholela kwa kutoa sababu zisizo za kuridhisha, kwa mfano kesi ya kundi la pili la wakufunzi wa walimu iliyokuwa ikitarajiwa kufanyika tarehe 10 Julai.

Kesi iliahirishwa kwa maombi ya wakala wa upande wa REB wakishindilia kwamba kifungo cha 140 cha sheria ya ajira kinaeleza kwamba mgogoro unaozuka kati ya mwajiri na mwajiriwa unatatuliwa kwanza na wajumbe wa wafanyakazi wa chuo kilichomwajiri wanaposhinwa kufikia makubaliyano ya pamoja wanapeleka kesi yao kwa mkaguzi mkuu wa masuala ya ajira na wanaposhindwa basi kuelewana mgogoro huo hutatuliwa kwa njia ya mahakama.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kesi hiyi ya wakufunzi wa walimu (wa Kingereza) ilianza mwaka wa 2015 ambako wakufunzi wa walimu 800 walifutwa kazi na idara ya taifa ya elimu (REB) kabla ya kandarasi yao kufikia mwisho.

Mpaka sasa wakufunzi wa walimu wapatao 200 ndio waliokwisha peleka madai yao mahakamani. Kwa mjibu wa sheria ya ajira wengine wana hadi tarehe 11 Julai kuasilisha madai yao kwa mkaguzi mkuu wa ajira. Kwa kuwa kesi ya madai ya ajira hayana maana kamwe baada ya miaka miwili.

Iwapo REB itapatikana na kosa kwa mjibu wa wakala wao mahakamani italazimika kulipa marupurupu yote yaliyokuwa akisalia kwenye kandarasi ya kila mkufunzi , fidia, na malipo mengine yaliyokuwemo kwenye kandarasi na hata wale wanaotoka nchi za kigeni kulipwa ada ya kusafiri. Zaidi ya hayo REB ingelazimu kulipa gharama ya kesi na hata marupurupu ya wakala.

Kufutwa kazi kwa wakufunzi hawa kulisababisha matatizo mengi yakiwemo kukosa kazi na hata kuathiri hali ya maisha ya familia zao.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.