kwamamaza 7

Kenya:Wanyarwanda na Warundi wakamatwa kwa kuishi kinyume na sheria

0

Wanyarwanda na Warundi  50  wamekamtwa na kurudishawa kwao kwa kutokua na vitambulisho vya kuishi humo kama inavyohakikishwa na ubalozi wa hizi nchi.

Wanaokamatwa ni wafanyakazi wa mambo ya kawaida kama vile washonaji, vinyozi na wengine ambao si rahisi kupata vitambulisho.

Serikali ya Kenya inafanya hili kwa kutekeleza amri ya waziri wake wa usalama, Fred Matiang’i ya kuomba polisi kuwatafuta wanaosihi nchini humo bila vitambulisho rasmi.

Balozi wa Rwanda nchini Kenya, James Kimonyo amewataka Wanyarwanda kufuata kanuni na sheria za kuishi nchini Kenya.

“ Tunakubaliana kwamba  ni umuhimu raia kutembeleleana lakini haina budi kufuata kanuni na  sheria. Suala hili tunalijadili kwa unyenyekevu ili wle wenye vitambulisho wasikose haki zao”

Balozi Kimonyo ametangazia VOA wanatafuta suluhisho la hili suala  la Wanyarwanda waliokamatwa.

Takwimu balozi wa Rwanda na Burundi zinaonyesha kwamba kuna Wanyarwanda na Warundi elfu nane nchini Kenya.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.