kwamamaza 7

Kenya: Balozi wa Rwanda James Kimonyo awaita vijana kukuza uzalendo

0

Balozi wa Rwanda katika nchi ya Kenya, James Kimonyo aliwaita vijana wa Rwanda wanaoishi Kenya kuchangia mno katika maendeleo ya nchi ya kizazi na kutosikiliza maadui wa nchi wanaotaka kuirudisha ilipotoka.

Kimonyo alisema katika mkutano wa wanyarwanda wanaoishi Kenya ambapo watu zaidi ya 500 walishirikia katika jumba la Kenyatta mjini Nairobi.

Aliwaita vijana kuwanyima muda wanaoenea siasa ya mgawanyiko. “Uongozi wa nchi yetu uliweka njia ya kujiundia kazi kwa kila raia hasa hasa vijana. Ni lazima kufanya bidii ili kuendelea badala ya kupoteza wakati katika mambo yasiokuwa na umuhimu wowote.”

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Katika mazungumzo yake, balozi alionyesha njia nchi ilipitia kuhusu umoja wa raia na maridhiano kwani nchi ilikuwa inakosa mabadiliko ya kisiasa, na ndio maana kuanzisha vita vya kuikomboa nchi mnamo 1994.

“Vita vya kuikomboa nchi vilikuwa na lengo la kukumbatia umoja wa nchi, kuendeleza demokrasia, usalama kwa wanyarwanda wote na kujenga uchumi imara pamoja na kuwarudisha nchini mwa kizazi wakimbizi. Mambo haya yote yalisababisha nchi kufika mahari inapokuwa, na vijana walishiriki katika vita vya kujikomboa.

Kabla ya kuwa balozi, James Kimonyo aliwahi kuwa Gavana wa mkoa wa zamani wa Kibungo ambao hivi leo unapatikana katika mkoa wa Mashariki, kati ya mwaka 2002 na 2004. Baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi Kimonyo alishikilia nyadhifa mbali mbali katika serikali ya mpito.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.