kwamamaza 7

Kayonza: Raia wana wasiwasi wa kuishi karibu kiboko aliemuua jirani wao

0

Raia wa sehemu ya Gitara, tarafa ya Kabare, wilaya ya Kayonza, wanasema kwamba wana wasiwasi wa kiboko anaeishi kwenye boma la kuzuia maji lilichimbwa kwa ajili ya kumwagilia mimea katika tarafa hiyo.

Wanasema kwamba inapofika jioni, kiboko huyo huvamia mashamba ya mimea yao. Habimana Gaspard ambaye ni mkazi wa tarafa hiyi, ameiambia bwiza.com kwamba kiboko huyu ni tatit kwa wakazi wa eneo hilo kwa kuwa alimuua raia mmoja na kuongeza kwamba kusingechukuliwa hatua kiboko huyo angewaua watu wengine.

“kiboko huyo anaishi katika bomu lile, anatufanya kuwa na wasiwasi kwa kuwa huwa tuna oga wa kila wakati, anatoka usiku akaenda mashambani kuharibu na kula mimea ama kuikanyaga kanyaga, anatufanya kuwa na wasiwasi kwa kuwa kuna raia mmoja alietoka Cyangugu kwa kusaka kazi ambaye ameuawa na kiboko huyu hivi karibuni. Tunaomba watafute jinsi ya kumfukuza kwa kuwa anatutesa kabsa, Kwa sasa tutafanya kila iwezekanavyo kulala mapema ili kiboko huyo asishambulie tukiwa hatujalala” alisema

Kageruka Venant ni mkazi mwingine anaesema amelemaa kwa sababu ya huyo kiboko, maisha yake yamo hatarini kwa kuwa na hata fedha walizolimpa kwa hasara hiyo hazikusaidia kitu.

“Hivi nimelemaa kwa sababu ya kiboko tuliyemkuta ikiwa ni saa tisa za usiku tukiwa kwenye doria ya kijiji chetu cha Kajevuba, wenzengu walikimbia na akanishambulia na nikadondoka kwenye mti, wenzangu wakapiga kelele na kiboko akakimbia kwa hofu ya kelele. Nilikwenda kutibiwa hospitali ya CHUK, ambako nilishinda miezi sita, hivi nimekwisha kuwa mlemavu, nategemea vitu vya kunishika nikitembea . Naomba msaada kwa kuwa nilishinda miezi 6 hospitali na hata fedha 1,715,000 ambayo nimelipwa na RDB iliishia kwa kulipa tiba na iliyokuwa inabaki nilimlipa alienitetea katika tatizo hili”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Murenzi Jean Claude, mayor wa wilaya ya Kayonza alisema kuwa tatizo hili la kiboko walilijadili mafisa wa wilaya wakishirikiana na ngazi husika

“Hebu, amekwisha hata hazaa, Hawakukwambia? Kwa ushirikiano na ngazi husika tulikwenda kumwinda , na hatukumgundua akikamatwa atarudishwa kwenye mbuga ya wanyama” Meya asema

Alipoulizwa juu ya mtu ambaye alilemaa kwa sababu ya kiboko huyu alisema kwamba hakufamu “ acha nitalifanyia uchunguzi suala hilo”

Hata hivyo, Jean Damascene Harelimana makamu meya wa wilaya anaejadili ustawi wa jamii, wakati alipojibu maswala ya mwandishi wa habari wa bwiza.com alimwambia kuwa yeye hana habari kamili na kumshauri kuuliza meya

Meya eti “ kiboko huyo akipatikana atarutishwa kwenye mbuga ya wanyama , katibu mutendaji eti “atafyatuliwa kwa risasi”

Katibu mtendaji wa tarafa ya Kabare, Jean Paul Kagabo, anakiri kwamba kiboko huyo akipatikana atafyatuliwa na kusisitiza kuwa na hata utawala wa mbuga ya wanyama ya Akagera uliidhinisha

“ni kweli kiboko huyo yupo tuliweka kundi la kujadili tatizo hilo na wakati wowote kiboko huyo atakapojitokeza tutamfyatua kwa risasi” asema

Mfanyakazi wa Mbuga ya wanyama ya Akagera, Karama anayehusika na uadifa wa kutatutua tatizo hilo, hakutaka kutoa habari juu ya tatizo hili. Inaonekana viongozi wanatofautiana kimaneno juu ya suluhu ya tatizo hili ambalo limedumu miaka miwili na kufanya raia kujiuliza kipi kilichokosekana ili kumaliza suala hili.

Hii si mara ya kwanza wakazi wa karibu na Mbuga ya wanyama ya Akagera kulalamikia wanyama wanaotoroka na kuja kula na kuharibu mimea yao. Na hili ni hususani dhidi ya raia wa wilaya ya Rwamagana na Gatsibo, wilaya ambazo hupakana na ziwa la Muhazi na Mbuga ya wanyama ya Akagera.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.