kwamamaza 7

Katika hotuba ya kuaga Rais Obama alizungumzia ubaguzi

0

Rais wa Marekani, Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho akiwa rais, akitoa hotuba hiyo katika mkusanyiko wa watu katika mji alikohamia wa Chicago.

Zaidi ya watu 20,000 walihudhuria hotuba hiyo ya kuaga, ambapo Obama alizungumza kuhusu ubaguzi, mafanikio yake kama rais na ulinzi wa mazingira.

[ad id=”72″]

Aliwashukuru waungaji wake mkono na kuzungumzia juu ya kusonga mbele kama taifa bora na imara. Obama amesema amejifunza kwamba mabadiliko yanaweza kutokea wakati watu wa kawaida watajihusisha katika masuala ya nchi.

Baada ya miaka minane ya kuwa rais, ameongeza kwamba anaamini na sio tu imani yake, lakini ni kutokana mawazo ya Wamarekani katika kujitawala.

Ni mtazamo kwamba kila binadamu ni sawa, kama alivyotuumba Mwenyezi Mungu kwa kuwa na haki maalum, kama vile uhai, uhuru na kuishi kwa furaha.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ataapishwa Januari 20 kushika madaraka ya rais.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.