kwamamaza 7

Karongi: Hawaelewi jinsi watajenga uwanja wa ndege na hawana kituo cha gari

0

Mwezi juni inatarajiwa kuanza kujenga uwanja wa ndege kwa ajili ya kuzua utali, wakaaji wamoja husema hawaoni umuhimu wa uwanja wa ndege kuliko kupata nafasi ya kungojea gari.

Wilaya hio ya Karongi ni tajiri kwa mambo ya utali ila ikiwa masikini katika mambo ya msingi kama barabara na mengine.

Pamoja na ushirikiano wa wilaya na Engineering Brigade wanakwenda kuanza tendo la majenzi la uwanja wa ndege na itakuwa moja ya suluhisho la kutokuwa na barabara.

Ila wakaaji wao huona kwamba uwanja wa ndege si lazima sana kwa kuwa hata watakao bahatika kutumia ndege hiyo ni wachache sana.

Erneste Kamanzi mfanya biashara ya mayai eti “hakuna anayeweza kukataa tendo la maendeleo likija, ila uchaguzi ungelikuwa kwangu mimi ningelichagua kituo cha magari kwani ndio usumbufu wetu”.

Hanyurwimana Jean Damacsene  anayehusika na barabara na vilalo na ndie atakaye husika na ujenzi wa uwanja anasema kua uwanja huo utaleta faida nyingi katika wilaya.

Akirudilia kituo cha gari alisema si lazima sana eti “watahitaji gari za kuwatwaa, hoteli na mengine, inaonekana kuwa raia watafaidika mengi”.

Aliendelea na kusema kuwa tayari barabara za kuelekea nafasi ya majenzi wa uwanja wa ndege zimeanza tengenezwa katika kiini cha Kiniha pamoja na Kibuye. Inatarajiwa kuwa mwisho wa mwaka huu majenzi yatamalizika na itachukua pesa zaidi ya miliyoni 51 pesa za Rwanda.

Wanaopendelea bwiza.com iwatembelee na kuwatangazia habari kwenye bidhaa vyao wanaweza kutumia ujumbe kwenye barua pepe ya meckypro@gmail.com, ama wapigie simu kwenye nambari ifuatayo: 0784685981.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.