kwamamaza 7

Kanombe:Hospitali ya kijeshi yapata mashine ya kuchunguza na kutibu kansa

0

Hospitali ya Kanombe imepokea mashine ambayo itasaidia kuchunguza na kutibu kansa kwa upesi kutokana na kuwa inaweza wa kutoa matokeo wakati wa siku tano badala ya kumi na tano.

Akizungumza na walaka ya utangaza nchini Rwanda(RBA), daktari Major Dr.Emile Kalinganile amefafanua kuwa mashine hii itawasaidia kupata matokeo kwa upesi kwa kuwa mashine hii inatumia mbinu za teknolojia za kisasa(digital pathology),amesema”Haisitahili kuenda CHUK ama Faysal ili kumpata daktari,tunatumia tekinolojia ya kisasa ili kutumia mda mfupi wa kumpa mgonjwa matokeo”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwenzake daktari,Lt.Col. Dr.Fabien Ntaganda amesema kwamba mashine hii itawasaidia  kuchunguza na kuganga aina zote za kansa hata katika damu au ile ya kawaida, pia kwa watoto na watu wazima.Hii ni hatua itakayowezekana kwa msaada wa madaktari bingwa kutoka Boston,marekani watakaosaidia  madaktari 14 kutoka Rwanda.

Mashine hii ni zawadi kutoka maoni ya rais  wa marekani miaka iliyopita,Barrack Obama ili kupambana na kansa,ina bei ya $100,000 kumaanisha miliyoni 85,000,000 frw

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.