kwamamaza 7

Kanali katika Jeshi la Rwanda aponea chupu chupu

0

Kanali  katika Jeshi la Rwanda (RDF), Sebowa Mishaki  jana alifanya ajali lakini akanusurika pamoja na dereva wake.

Imeripotiwa ajali hiyo imetokea Wilayani Nyamagabe Kusini magharibi mwa Rwanda na wawili wamejeruhiwa.

Mashahidi wamesema wamesema inawezekana kuwa gari lilkuwa na mwendo wa kasi kwenye barabara linaloshuka.

Kanali Mishaki amelazwa Hospitalini Kanombe, Mjini Kigali na dereva wake anatibiwa hospitalini Mjini Butare, kusini mwa Rwanda.

Msemaji wa Polisi ya Usalama wa Barabarani, Jean Marie Vianney Ndushabandi amesema hajajua kwa mapana na malefu kuhusu ajali hii.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.