kwamamaza 7

Kampeni za Kagame zafikia mwisho – awalaumu waliopinga ugombea wake

0

Siku ya leo tarehe 2 Agosti ikiwa inasalia masaa machache kura kupigwa mgombea wa RPF, Paul Kagame aendesha kampeni zake za mwisho ambazo zimefanyika wilaya ya Gasabo mjini Kigali.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katika hafla hiyi ambako kulikuwa na wananchi wengi na hata viongozi wakuu wa ngazi mbalimbali ambapo wenyekiti wa vyama vilivyojiunga na RPF nao walipewa fursa ya kuhotubia kwa wananchi walioshiriki hafla hiyo. Hawa ni pamoja na Vicent Biruta mwenyekiti wa PSD, Mukabaranga Agnes mwenyekiti wa chama cha PDC, Sheikh Mussa Fazil Harerimana mwenyekiti wa chama cha PDI.

Waziri Kabarebe
seneta Rutaremara

Mgombea huyu ambaye amekuwa akifanya ziara ya mwisho ya kampeni zake wilaya ya Gasabo aliwaambia wananchi kwamba anafurahia jinsi kampeni zilivyokuwa hata hivyo hakukosa kuwagusia viongozi wa nchi za magharibi waliotamka juu ya ugombea wake na hasa serekali yake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“hapo mwanzo wa kampeni Ruhango kuna maneno niliyoyasema, na watu wakatoa maoni ya kutulaumu na baada ya kuona kwamba hayazai matunda wakasema ‘ Rwanda itakuwa na usalama baada ya utawala wa Kagame?’ niwaulize kitu kimoja kabla ya kushika utawala ilikuwa vipi?”

“Wanasema ndio walioileta demokrasi, ndio wanaoihamasisha lakini hivi karibuni waliingia kitendo cha kuashiria demokrasi na baadaye wakasema mambo hayakuenda vizuri kwa kuwa walituingilia mifumo ya mtandao na kudukua kura” aliendelea kusema

Unaifundisha demokrasi kivipi ikiwa na mambo yako hayakuenda vizuri, kompyuta ilikuchagulia rais kivipi?.

Paul Kagame aliendelea kuwaelezea kuwa uchaguzi wa tarehe 4 utakuwa ishara ya pale wanyarwanda wanapotaka kuelekea ambapo watakuwa wakichagua wakilenga kuwa na viongozi wenye kutekeleza wajibu wao kulingana na mwendo wa utawala bora.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.