kwamamaza 7

Kampeni mgombea Frank za mwisho zilizofanyika Nyarugenge zakuwa fahari

0

Jana ikiwa ni tarehe 2 Agosti, masaa machache kabla ya uchaguzi rasmi kutimua vumbi, mgombea wa chama cha Green Dkt. Frank Habineza afanya kampeni zake za mwisho ambazo zimehudhuriwa na watu wengi kuliko siku yoyote nyingine ya kampeni zake.

Kampeni zake kwa siku ya 19 ambayo ndiyo siku ya mwisho zimefanyika wilaya ya Nyarugenge eneo la Nyabugogo.

Alipokuwa akihotubia wa wanchi waliokuja kusikia sera zake aligusia kuhusu ziara zake za kampeni za awali kutoka mwanzo hadi mwisho na kugusia kuhusu pingamizi alizokutana nazo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Aliwashkuru pia waliomsaidia katika ziara yake nzima ya uchaguzi. Kulingana na maneno yake, jinsi ambayo kampeni zake zilifanyika ni imani kwake kushinda uchaguzi.

Aliwapa moyo wafanyabiashara wa eneo la Nyabugogo baada ya kusema kuwa atawaacha wakaendeshe biashara yao kulingana na matakwa yao.

“Kabla ya mwezi wa tisa kumalizika kila yeyote anayeendesha biashara atakuwa na uhuru wa kuendesha biashara bila wasiwasi wowote ,wafanyabiashara wafanye, waendesha magari waendeshe na kadhalika.

Hapa pia aliwaahidi kwamba iwapo atachaguliwa atayafunga magereza yasiyo halali kisheria kama gereza ya Gikondo ambayo inafahamika kama Kwa Kabuga.

Dkt. Frank ni mgombea kwa tiketi ya chama cha Green na anawania kiti cha urais pamoja na wagombea tatu ambao ni Paul Kagame wa chama cha RPF na hata Phillipe Mpayimana ambaye ndiye mgombea huru pekee aliyewahi kuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi ya Rwanda.

Uchaguzi unatarajiwa kuanza leo hii tarehe 3 kwa wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi na tarehe 4 kwa wanyarwanda wa ndani ya nchi.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.