Swahili
HABARI

Kamonyi:Walimu walalamika kwa kutopata ziada

Walimu kutoka wilaya ya  Kamonyi wanasema kuwa wilaya haijawapatia fedha za ziada za mwaka huu ilizokubalia walimu wanaotimiza lengo la kazi na la ushindi wa wanafunzi.

Wakizungumza na Bwiza.com wamesema kuwa wilaya haijalipa fedha za ziada za mwaka huu unaokaribia kwenye mwisho wa bajeti yake.Mmoja wao amesema  kuwa walikosa mtu wa kuuliza tatizo lao kwa kuwa na wakurugenzi wanawambia kuwa hawana habari yoyote kuhusu fedha hizi,mmoja amesema”Tunasubiri lakini hatujui tunamsubirio nani ”.

Wenzake wameleza kuwa wanazoea kupata ziada  mwezi June kabla ya mwanzo wa mwaka wa bajeti mwingine, kwa hiyo wanashangaa kuona kwamba wanafika mwisho wa mwezi wa Agosti bado hawajapata fedha hizi na kuongeza kuwa ni vigumu kutimiza lengo kwa kuwa hawana vitabu vya kutosha hasa vya lugha ya Kifaransa na Kinyarwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Akiongea kuhusu malalamishi ya walimu hawa,Ofisa kwa wajibu wa mishahara wa wilaya ya Kamonyi,Vestine Mukansigaye kupitia simu amefafanua kuwa kulikuweko kuchelewa kulipa kwa sababu walichelewa kuzipata alama za wanafunzi  kwa hiyo fedha hazikuchelewa.Vestine amesema”Nilimaliza kazi yangu na ankara zimeisha tumwa kwenye wizara ya mali na usimamizi”.

Kiongozi huyu ameongeza kuwa bilashaka kesho au kesho kutwa watapata fedha zao za ziada za mwaka wa 2017

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com