Kulizuka vurugu na hali ya mshikemshike katika kanisa moja katika mtaa huu wa Kashani, Mombasa kahaba aliyeokoka alipowataja baadhi ya waumini wa kanisa hilo akiwemo pasta baba mchungaji kuwa baadhi ya wateja wake wa hapo awali.

Penyenye zaeleza kuwa dada huyo aliyeokoka hivi majuzi alitakiwa kutoa ushuhuda ili kuweka nafsi yake huru dhidi ya vitendo vyake vya awali vilivyoenda kinyume cha dini.

Kwanza, kidosho huyo alisita kufanya kama alivyoagizwa pengine akihofia kuchafua hali ya amani. Hata hivyo, baada ya shinikizo kutoka kwa mama wa kanisa aliyemsimamia wakati wake wa kuokoka, aliamua kutoa ushuhuda wake.

Kwa mshangao wa wengi, aliwataja pasta mkuu, msaidizi wake na wazee wawili wa kanisa hilo kama baadhi ya waliokuwa wateja wake wakati alipokuwa akiimudu biashara ya kuchuuza uroda.

Huku akishangiliwa na baadhi ya vijana kwa nduru za, “toboa dada toboa” dada huyo alisimulia jinsi wateja wake walivyomjia usiku na hata kiasi cha fedha alizo walipisha.

Suala hilo lilizua hali ya sintofahamu ikizingatiwa kuwa pasta mkuu na mdogo wake walikuwa baadhi ya waliotajwa. Vijana walipiga nduru wakitaka waliotajwa kuondoka kanisani mara moja au wawaonyeshe cha mtema kuni. Ilibidi ibada ikatizwe siku hiyo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.