kwamamaza 7

Kagame yashinda baado akiwazidi kwa pengo kubwa wagombea wenzake

0

Katika jioni ya siku ya leo tarehe 4 Agosti ndipo Tume ya Uchaguzi ilipotangaza matokeo ya muda ya kura zote ambapo Kagame Paul anazidi kuwashinda kwa kishindo wagombea wenza ambao hakuna hata mmoja aliyewahi kupata hata asilimia moja.

Kulingana na matokeo hayo Kagame Paul ndiye aliyeshinda kwa kishindo cha asilimia 98.63 akifuatiwa na Mpayimana Philippe na asilimia 0.73 halafu  Frank Habineza na asilimia 0.47.

Matokeo hayo ni kutoka kwa jumla ya wapiga kura 6,897,076 waliopigia kura kwenye vituo vya uchaguzi 2,340 vya wilaya zote za nchi.

Baada ya uchaguzi huu wagombea ambao hawakuweza kushinda walikubali matokeo ambapo Mpayimana Philippe alisema kuwa anaheshimu maoni ya wanyarwanda na kwamba ataendelea na mipango yake kwa madhumuni ya kudumisha demokrasi.

Hatimaye Frank Habineza naye alikubali matokeo na kusema licha ya kuwa walizikuta pingamizi kadhaa hawajakata tama kwa kuwa nja ya kupambania demokrasi ingali ndefu.

Paul Kagame ambaye ameshinda uchaguzi huu atashika kiti cha urais kwa muhula wa miaka saba na ambako kulingana na mabadiliko yaliyofanyiwa katiba kufuatia kura ya maoni ya 2015, rais huyo anaweza kuwania mihula yote miwili ijayo ambapo anaweza kuongoza hadi mwaka 2034.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.