kwamamaza 7

Kagame aendesha kampeni mbili wilaya ya Gicumbi

0

Mgombea wa chama cha RPF, Paul Kagame jana tarehe 1 Agosti  amekuwa wilaya ya Gicumbi iliyoko jimbo la kaskazini ambako ameendesha kampeni mbili ya kwanza kwenye tarafa ya Cyumba na baadaye kwenye tarafa ya Rutare .

Hapa wananchi walikuwa wengi kumpokea rais Kagame kama ilivyokuwa kwenye kampeni za awali katika wilaya Nyingine alizozipitia.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rais Kagame alipokuwa tarafa ya Cyumba aliwaahidi wananchi wa Byumba kwamba safari ya kuijenga nchi inaendelea na sera nzuri na hata miundombinu zitazidi kuwafikia.

“tumejifunza mengi, tulipotoka, njia tuliyoipitia ilitufunza mengi, hapa natilia mkazo kwa Gicumbi kwa kuwa ina historia yake iliyo sawa na ya wanyarwanda wengine hasahasa kwa kuibadili nchi”

 

Amesema kuwa tarehe 4 ambapo ndipo uchaguzi mkuu utakapopigwa ina maana muhimu katika siku zijazo za nchi.

“ina maana ya umoja, maendeleo, haki ya kila mnyarwanda, chaguo linalomstahili mnyarwanda, linaloistahili Rwanda, Gicumbi inaifaa Rwanda, wanyarwanda wote wanaifaa Rwanda”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Amesema kwamba waliyoyafikia yote ni kupitia ushirikiano uliowasifu wanyarwanda kutoka miaka mingi iliyopita.

Alipomaliza shughuli zake hapo aliendelea kwenye tarafa ya Cyumba hapo aligusia mambo mengi kuhusu historia waliyoipitia na yale waliyoyafikia kwamba yote ni kwa ajili ya ushirikiano wa wanyarwanda.

“Miaka imekuwa ishirini na zaidi tukiwa pamoja tukijijenga, tukiijenga nchi yetu, takiujenga usalama, maendeleo, umoja ,miundombinu, shule, hospitali, barabara, n.k. tumeyafikia mengi lakini safari ingali baado ndefu, tunaendelea katika safari ya kujiendeleza” asema

Ameongeza “hatungeweza kufika mbali bila kuwa pamoja, bila kushirikiana, kufanya kazi, bila kufuata njia ya siasa nzuri inayojenga ;maji, na vingine vingali pungufu lakini katika miaka 7 itakayokuja kama mlivyochagua mambo yatakuwa mazuri mno, na mtayafikia mengi”

Aliwakumbusha kwamba tarehe nne ndio ya kuamua kuendelea safari hiyo ya kujijenga, watu wakapata maji safi, vijana wakaendelea kupewa fursa za kujiendeleza, watoto wakapewa elmu nzuri, wanawake na wanaume wote wakaendelea kujiendeleza bila yeyote kuachiwa nyuma, wafanyabiashara wakapata faida na wakawekeza mtaji katika miradi wanayoitaka.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.