kwamamaza 7

Jua mengi kuhusu mchango wa Uganda katika vita baridi vinavyosemekana kuweko kati yake na Rwanda

0

Taarifa za Chimpreports wiki iliyopita ziliweka wazi kuweko vita baridi kati ya Rwanda na Uganda. Hata hivyo,mambo yamekuenda mkia wa mbuzi   baada ya kumkamata Rene Rutagungira na kumshtaki kumteka nyara aliyewahi kuwa mlinzi wa Rais Kagame,Luteni Joel Mutabazi aliyehukumiwa kufungwa maisha jela.

Hata kama mafisa wa pande mbili hawajatangaza hadaharani lolote kuhusu vita baridi hivi,kuna mambo yaliyotokea hasa kwa upande wa Uganda miaka iliyopita ambayo hayakufurahisha Rwanda na yalizusha kutoelewana kati ya nchi hizi.

Taarifa za The East African,asili ya habari hii,zimeorodhesha matukio yafuatayo:

Mnamo mwaka 2015, Uganda na Rwanda walikubaliana kuwapa mahali pa kuishi wakimbizi asili ya Eritrea waliokuweko nchini Israel.Jambo hili lilifanywa na ofisi ya upelelezi ya Israel,Mossad.Baada ya haya Waziri wa ushirikiano na nje wa Uganda, Philemon Mateke alimuita Barozi wa Rwanda kwa Uganda,Frank Mugambage na kudai kwamba Rwanda imeanza kutoa ardhi ya Uganda kwa idadi ya wakimbizi iliyokubali kukaribisha.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa mjbu wa afisa husika na kisa hiki,a Uganda haikutaka utoaji wa suluhisho wa jambo hili hata kama Rwanda ilipendekeza kuanzisha kamati ya kujadili suala hili.

Pia,Uganda inasemekana kuwateua mafisa ambao ni maadui wakubwa kwa serikali ya Rwanda.

Taarifa hizi zimetoa mfano wa uteuzi wa Brig.Francis Kaka kwenye nafasi ya uongozi mkuu wa bodi ya usalama wa ndani nchini Uganda kwa kuchukua nafasi ya Brig.Ronald Barya.Inasemekana kuwa Kaka  ni rafiki wa dhati wa ami ya Rais Museveni,Gen.Caleb Akandwanaho anayejulikana kama Salem Saleh ambaye hana ushirikiano mzuri na serikali ya Rwanda.

Pia uteuzi wa Gen.Henry Tumukunde kama waziri wa usalama na wa Abel Kandiho kama kiongozi wa upelelezi wa kijeshi ambao hawaelewani na serikali ya Rwanda kuliharibu ushirikiano.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Jambo ni jingine ni ziara ya binti malehemu, mpelelezi Patrick Karegeya,Portia Mbabazi Karegeya.Msichana huyu ilikuwa vigumu kukaribishwa kwenye uwanja wa ndege mjini Kampala, lakini mafisa wakuu wa Uganda waliwezesha hili kinyume na ombi la serikali ya Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hatimaye kuna miradi mbalimbali husika na uchumi,miundo mbinu ambayo Uganda ilienda goigoi kutia kivitendo na kuwa Uganda ilionyesha uvivu wa kuwatuma watuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwana 1994 wanaoishi nchini Uganda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya, ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda unasemekana kuwa katika vita baridi wakati ambapo kulikuwa mwanga mzuri wa ushirikiano mzuri mwaka 2011 ambapo marais wa nchi hizi mbili walikuwa wakitembeleana.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.