Swahili
HABARI MPYA

Jose Chameleone ashtakiwa kuharibu mkataba wa  Shilingi miliyoni 53

Muimbaji Dr.Jose Chameleone

Mwanamke kwa jina la Zaina Muwonge amemshtaki mahakamani muimbaji Joseph Mayanja maarufu kama  Dr.Jose Chameleone  juu  ya kushindwa kufanya tamasha nchini Afrika Kusini ambapo alipokea Shiling za Uganda miliyoni 53.

Zaina Muwonge jana  amejulisha mahakama kwamba alikubaliana na Jose Chameleone kufanya tamasha kwa jina la “Wale wale”mwaka 2015.

Taarifa za Dailymonitor zimeeleza kuwa  Zaina Muwonge amesema kwamba aliwasiliana na Jose Chameleone kuhusu tamasha hii ambayo ilitarajiwa kufanyika mjini Durban,East Durban,Pretoria na Cape.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Zaina Muwonge ameongeza kwamba Jose Chameleone alimuambia kwamba hatakuja kwa kuwa vitambulisho vilibiwa kisha  huyu muimbaji akampigia simu mwaka 2016 akimuomba msamaha jambo lilomfanya kufanya maandalizi ya tamasha nyinge ambayo Chameleone hakufanya baada ya kufunga simu yake siku moja kabla kupanda ndege kuelekea nchini Afrika kusini.

Kupitia wanasheria Lukwago and Company advocates,Zaina Muwonge anamtaka Chameleone Kumrudisha fedha zake na kulipa fidia ya yaliyoharibika juu ya kuharibu mkataba,jina na mali yake.

  Bonyeza BWIZA TV kupata habari  na nyimbo mpya

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com