kwamamaza 7

Jeshi na polisi vya Uganda vyafunguka kuhusu vitendo vya kuwakamata Wanyarwanda

0

Baada ya Rwanda kuitaka serikali ya Uganda kueleza mengi zaidi  kuhusu vitendo vya kuwakamata Wanyarwanda,jeshi na polisi vya Uganda vimetoa mawazo yake kuhusu vitendo hivi.

Msemaji wa jeshi la Uganda,Brig.Gen. Richard Karemire akizungumza na NTV,amehakikisha kwamba wizara ya mambo ya nje ilipokea barua ya Rwanda husika.

Brig.Gen.Richard Karemire ameeleza kwamba suala la watu  waliokataliwa kuwasiliana na wanasheria  wao watasaidiwa kwa ushirikiano na wanausalama wengine nchini ili kujua walipofungiwa,matatizo yao na kuongeza kwamba watapatiwa haki zao vilivyo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waliokamatwa na kutoweka kuna James Bayingana, Lando Alice Kabano, Vianney Byaruhanga, Herbert Munyangaju, Freddy Turatsinze, Jessica Muhongerwa, Vanessa Gasaro, Diane Kamikazi na Diane Kamashazi.

Mmoja mwa Wanasheria wao,Gawaya Tegulle amesema kwamba hata kama ushirikikiano kati ya Rwanda na Uganda siyo bora kukiuka haki za binadamu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande wa polisi kupitia msemaji wake,Emilian Kayima ametangaza kuwa hakuna ripoti yoyote ya kituo cha polisi inayoonyesha kwamba   watu waliotajwa  ni wafungwa gerezani nchini Uganda.

Pamoja na haya,ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda umendelea kuwa mkia wa mbuzi tangu mwezi Otoba 2017 baada ya kumkamata Mnyarwanda Rene Rutagungira kwa kumshitaki kuwa mpelelzi wa Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.