Swahili
Home » Jeshi la Uganda lilivyomsaidia Rais Nkurunziza kurudi Burundi baada ya kupinduliwa
HABARI MPYA

Jeshi la Uganda lilivyomsaidia Rais Nkurunziza kurudi Burundi baada ya kupinduliwa

Imejuliakana namna ambavyo  Jeshi la Uganda (UPDF)  lilimsaidia mno Rais Pierre Nkurunziza baada ya Jen.Godfrey Niyombare kutangaza ameupindua uongozi wake tarehe 13 Meyi mwaka 2015.

Rais Nkurunziza aliyekuwa nchini Tanzania kwa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki alipata msaada huu kwa amri ya Rais Museveni.

Rais Museveni alimuita mmoja mwa viongozi wa jeshi, Brig. Sabiiti Muzeeyi na kumpa amri ya kuwachagua wanajeshi mahiri watakaosindikiza Rais Nkurunziza nchini Burundi.

Brig. Sabiiti Mugenyi aliyemsindikiza Rais Nkurunziza

Miongoni mwa waliochaguliwa  kuna wanajeshi waliokuwa katika vita nchini Somalia, Elite Commando 2 waliofanya mazoezi yao katika misitu ya huko wilayani Lira nchini Uganda kama inavyohakikishwa na chombo cha habari nchini Rwanda.

Kundi hili lilifanya kazi yake vizuri na kumrudisha Nkurunziza madarakani.

Kuna taarifa kwamba wengi mwao walibaki nchini Burundi kumlinda Rais Nkurunziza.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com