kwamamaza 7

Jeshi la Rwanda wameanza juma ijulikanayo kwa jina Army week

0

Jeshi la Rwanda wameandaa tena tendo lijulikanalo kwa jina Army week wakiyafanya mambo tofauti kwa ajili ya kuwasaidia raia maskini kwa kuwa na maisha mema ili kuachana na umaskini.

Kwa kuanjisha juma hio “Army Week” , jeshi walishirikiana na raia jana tarehe 4 Mei 2017 katika wilaya ya Kichukiro, tarafa ya Nyarugunga wakiwa katika tingitingi inayo husika na ulimaji wa mboga.

Jemadari mkuu wa Jeshi la Rwanda, Gen. Patrick Nyamvumba, husema kwamba matendo ya “Army Week” huonyesha kujikomboa ya ukweli kwa kuendeleza maisha mema ya raia kupitia msaada ya Wanyarwanda.

Katika tendo la wiki hii kutakuwemo matibabu ya magonjwa tofauti bila malipo, kujenga upya mambo ya msingi na mengine.

Msemaji wa jeshi la Rwanda, Lt. Col. Réné Ngendahimana, alisema kuwa wiki hii ni tofauti na miaka nyingine kwa sababu itakuwa kujali nchi yote, kwa sababu mbele ilikuwa wakihusika na wilaya moja au sehemu moja, itachukuwa muda murefu, ilianza tarehe 4 Mei na itafikia mwisho Julai 2017.

Waziri wa mambo ya msingi, Musoni James, alisema kuwa uongozi bora katika matendo kama haya ya “Army week”, jeshi wakishirikiana na raia kwa kujenga nguvu kwa ajili ya kutatua mambo tofauti ni bora zaidi.

Jeshi la Rwanda hawahusiki na kulinda usalama wa Rwanda pekee ila wanajali pia maendeleo kupitia matendo ya maendeleo ya raia.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Leki/bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.