kwamamaza 7

Jeshi la Rwanda lawashauri wananchi kutotafuta huduma nchini Uganda

0

Kiongozi wa Jeshi la Rwanda, Jen. Patrick Nyamvumba amewashauri wananchi wa karibu na mipaka na Uganda kutokwenda nchini humo kutafuta huduma.

Ujumbe huu umetolewa wakati ambapo Jeshi la Rwanda limeanzisha mpango wa kuwatibu wananchi ambako 800 Wilayani Burera walitibiwa ugonjwa  kama vile wa macho, meno n.k.

Jen. Nyamvumba amewambia wananchi huko kaskazini kwamba serikali inawaletea karibu huduma walizokuwa wakitafuta nchini Uganda na kuwataka kusubiri zile ambazo hawajapata bado.

“ Najua kwamba kuna wale ambao walikuwa wakitafuta huduma nchini jirani. Hakuna sababu ya kutafuta huduma nchini Uganda. Zinawaletewa karibu kwa kuwa inastahili. Inatugusa mnapoteswa kimwili.” Jen. Nyamvumba amesema

Pamoja na hayo, kwa kawaida wananchi wanaoishi karibu na mipaka na Uganda walikuwa wakipata hudumba mbalimbali nchini humo kama vile uganga, vyakula elimu, biashara, n.k.

 

.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.