Swahili
Home » Jeshi la Rwanda lawaonya wanaotaka kushambulia nchi kutoka DR Congo
HABARI MPYA

Jeshi la Rwanda lawaonya wanaotaka kushambulia nchi kutoka DR Congo

Jeshi la  Rwanda limewaonya wanaotaka kushambulia nchi kwa kutumia njia za vichochoro kati ya Rwanda na DR Congo.

Kiongozi wa brigedi ya 201, Kanuni Pascal Muhizi akizungumza na wakazi wa tarafa ya Rubavu kuhusu usalama, amewahamasisha  kutowaunga mkono watu wanaolenga kuharibu usalama wao.

Kiongozi wa brigedi ya 201, Kanuni Pascal Muhizi

“ Jeshi la Rwanda liko tayari kulinda usalama. Tatizo ni wale ambao watakuja kupitia njia za panya na nyinyi mkawapa mahali pa kukaa. Kuna habari kwamba kuna wale ambao wanataka kujaribu na hatuwezi kuzuia watu wanaotaka kujiua wenyewe”

“ Hatutaki ugomvi wowote na wakazi, ukitaka nyumbani kwako kuwa ‘military Camp’ ni kumpa makazi mhalifu” Kanuni Muhizi ameongeza.

Kanuni Muhizi amesistiza kuna wahalifu walio huko maeneo ya Rusayo na Nyiragongo ambao wanaweza kuja nchini Rwanda kuharibu usalama.

Jeshi limetangaza haya  baada ya mashambulizi yaliojitokeza mala mbili kwenye mpaka wa Rwanda  Burundi na kuwaua watu wawili,uwizi wa mali na mengine.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com