kwamamaza 7

Jeshi la Rwanda lafunguka “ Kuna maadui nchini Burundi na DR Congo”

0

Jeshi la Rwanda mkoa magharibi kusini wiki iliyopita  lilidai hakuna vita nchini Rwanda na kuwajulisha wakazi kuna maadui wa nchi nchini DR Congo na Burundi.

Kwenye mazungumzo na wakazi Wilyani Rusizi, Jen. Alexis Kagame  ambaye ni Kiongozi wa jeshi huko, amehamasiasha wakazi kuendelea na kazi zao za kila siku kwa kuwa  hakuna suala la usalama na kutolegeza kwa kuwa adui yupo nchini Burundi na DR Congo.

Jen. Alexis Kagame

“ Ni vizuri kwa kila mtu kuchunguza kama kuna watu wanaoweza kuharibu usalama. Hatuwezi kuficha hayo, kuna waliofanya uhalifu nchini humu ambao wangali nchini DR Congo. Kuna FDLR na CNRD. Kuna wanaotumia Burundi na wengine kutumia DR Congo” Jen. Kagame alisema

Jen. kagame alisema kuna fununu za vita  kutokana na yaliyotokea Wilayani Nyaruguru, kusini mwa nchi  ambako  wanamgambo wa FLN walijigamba kushambulia.

“ Mambo ni shwali…hakuna woga kwa wakazi,kuna fununu kwenye mitandao lakini kuna usalama kutoka Rubavu hadi huku” Jen. Kagame aliongeza

Akitoa hoja zake kuhusu Msemaji wa Jeshi la FLN, Meja Sankara Nsabimana,  Gavana wa Mkoa wa magharibi, Alphonse Munyentwari alisema kutoa mchango wao kupiga marufuku madai ya wanaolenga kushambulia nchi.

Gavana wa Mkoa wa Mgharibi, Alphonse Munyentwari

“ Mtu anawezaje kusema kwamba ametawala kipande cha nchi.Hatutakwepa fununu zinazotuhusu, Cha muhimu ni kupinga hizi fununu”  Gavana Munyentwari alisema

Haya ni baada ya wanamgambo wa FLN  tarehe 19 Juni 2018 kutoka upande wa mbuga ya Nyungwe, upande wa Burundi kushambulia Wilayani Nyaruguru. Hawa waliua watu wawili na kuwajeruhi wengine sita wakiwemo Katibu Mtendaji wa Tarafa ya Nyabimata, Vincent Nsengiyumva.

 

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.