kwamamaza 7

Jeshi la Rwanda lafunguka kuhusu ‘majigambo’ ya waliodai kushambulia Rwanda

0

Kiongozi wa Jeshi la Rwanda (RDF) mkoani Kusini, Meja Jen. Emmanuel Ruvusha  ametangaza madai ya kuwa kuna wanamgambo walioshambulia kusini mwa Rwanda wilayani Nyaruguru ni uongo mtupu.

Huyu mwanajeshi jana tarehe nane Ogasti mwaka huu amesema waliyosema wanamgambo kupitia vyombo vya habari vya kimataifa na mitandao ya kijamii ni uongo.

“ Ninachowaambia ni kwamba kuna usalama 100% katika mkoa wetu. Kuna wahalifu waliokuja kuharibu usalama wilayani Nyaruguru lakini suala hili limesuluhishwa na wanafanya kazi zao kila siku” Jen. Ruvusha ameeleza

Jen. Ruvusha ameongeza haikuwa mapambano ila hawa wahalifu walitilia nguvu madai yao na kuwa waakazi wanastahili kutowatega masikio.

Kwa upande mwingine,msemaji wa wanamgambo walioshambulia kwa jina la FLN, Meja Callixte Sankara alisema kuwa walipambana na jeshi la Rwanda mwezi mzima katika msitu wa Nyungwe karibu na Burundi.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.