Swahili
Home » Jeshi la Rwanda lafunguka kuhusu madai ya mashambulizi kaskazini magharibi
HABARI MPYA

Jeshi la Rwanda lafunguka kuhusu madai ya mashambulizi kaskazini magharibi

Kiongozi wa RDF wilayani Nyabihu na Rubavu

Kiongozi wa jeshi la Rwanda ( RDF) wilayani Rubavu na Naybihu, Kanuni Pascal Muhizi amewaambia wakazi jeshi lingali tayari kulinda usalama kwenye mipaka ya Rwanda na DR Congo.

Kanuni Muhizi amewataka wakazi kutowatega masikio wanaolenga kuharibu usalama wan chi.

“Kwa suala la usalama, sisi kutoka hapa hadi kule wilayani Musanze, usalama ni asilimia 100. Hakuna tatizo”

Huyu wanajeshi amehakikishia wakazi kwamba maeneo yote ambayo inawezekana kwa maadui kutumia yako chini ya ulinzi.

Pia Muhizi amewahamasisha wakazi kuwasiliana na wanausalama kwa  kuwapasha habari  ili kukamilisha ulinzi.

Siku zlizopita,maeneo  ya kaskazini magharibi nchini Rwanda kulijitokeza makundi ya watu wenye silaha kuingia kutoka nchini DR Congo na kuharibu usalama.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com