kwamamaza 7

Jeshi la Rwanda ladaiwa kuingia nchini Uganda

0

Taarifa kutoka nchini Uganda ni kwamba wanajeshi wa Rwanda wanaochunga usalama maeneo ya mpakani wanaingia nchini Uganda.

Kwa mujibu wa Chimpreports hawa wanajeshi wanakwenda nchini Uganda Wilayani Kisoro  kutafuta chakula, vinywaji na sigara.

Mmoja mwa wananchi Wilayani humo ambaye anauza chakula na vinywaji, Hellen Mwiza amehakikisha hizi taarifa.

“ Wanajeshi wa Rwanda huja wakiwa na bunduki na risasi na kunywa pombe, kula chakula kisha wakarudi kwao.”

Kwa upande wa Rwanda, kiongozi mmoja ambaye hakutaka jina lake lijulikane amesema “ Haiwezekani wanajeshi wa Rwanda kwenda nchini Uganda kutafuta chakula na vinywaji. Hawana sababu ya kufanya hayo.”

Bwiza.com imewasiliana na Msemaji wa Jeshi la Rwanda ili kujua msimamo wao kuhusu madai haya, lakini akakataa kutoa maelezo husika kwa kusema hawezi kueleza kila taarifa za vyombo vya habari.

Hata hivyo, wengi wamekosoa taarifa hizo kwa kudai zinalenga kupaka masizi Jeshi la Rwanda.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.